Posts

Showing posts from November 26, 2015

FAHAMU HAYA KUMI (10) KUHUSU BUSHMAN, “STAR WA GODS MUST BE CRAZY”.

Image
1. Ni nyota wa filamu ya “Gods must be crazy”, na jina lake kamili ni  N!xau  na ni maarufu duniani kwa jina la “ Bushman ”. 2. Ni raia wa  Namibia , Hakumbuki tarehe yake ya kuzaliwa na alifariki mnamo  mwaka 2003. Alikadiliwa kuwa amezaliwa mnamo  mwaka 1943. 3. Aliweza kuhesabu 1 – 20 tu na ndio maana alifuga mifugo ipatayo 20 na hakutaka kuzidisha zaidi ya hapo 4. Ni baba wa watoto 6 na wake 2, na familia yake ipo nchini kwake Namibia. 5. Ameigiza filamu saba (7) ambazo ni  i.The Gods Must Be Crazy (1980) ii.The Gods Must Be Crazy II (1988) iii. Kwacca Strikes Back (1990) iv.Crazy Safari (1991) v.Crazy Hong Kong (1993) vi.T he Gods Must be Funny in China (1994) vii.Sekai Ururun Taizaiki (1996) 6. Katika filamu yake ya kwanza aliambulia kiasi cha  shilingi 480,000 . kwa sababu katika kijiji chake walichokuwa wakiishi hawakuwa wakitumia pesa na aliona kama hazina umuhimu. 7. Baada ya kufundishwa umuhimu wa pesa ndipo...

Kidoa Wa "Akadumba" Akomaa na Madairekta Wapenda Ngono

Image
VIDEO Queen wa Ngoma ya Akadumba, Asha Salum ‘Kidoa’ amewakomalia madairekta wa filamu Bongo wanaopenda ngono kisha watoe kazi kuwa hatakubaliananao kirahisi na kwamba kwake ni kazi tu. Akipiga stori mbili-tatu na kona ya Bongo Movies, Kidoa ambaye kwa sasa ameingia katika filamu rasmi amesema kuwa, madairekta wengi Bongo wanaendekeza sana ngono ndiyo wampe mtu nafasi katika kucheza filamu jambo ambalo hatakubali limtokee. “Nimekutana na madairekta wengi wanaoendekeza ngono kwenye kazi. Sasa nimeshaingia kwenye filamu hivyo madairekta uchwara wataisoma namba maana hapa kwangu ni kazi tu na si vinginevyo,” alisema Kidoa.

RIHANNA , YOUNG THUG KUTOKA NA NGOMA YA PAMOJA

Image
Star wa kike wa muziki Duniani Rihanna na Star wa Hip hop Young Thug, wameingia studio pamoja ili kuulasimisha ‘mkwaju’ wa pamoja.  Rihanna ambaye anatarajia kuachia album yake ijumaa hii, bila shaka ngoma hii haiwezi kujumuishwa kwenye album hiyo kwa kuwa tayari ni ‘too late’.  Pengine wimbo huo utajumuishwa kwenye project inayofuata ya Young Thug, au itatoka kama pini la kujitegemea.  Mmoja kati ya watu walio kwenye uongozi wa rapper huyo, alivujisha picha ya wawili hao wakiwa studio na kuipa ‘Caption’ ya ‘Thug na Riri in the studio, kitu kikubwa kinakuja’.

Swagga za linnah Sanga zawachengua wabongo

Image
Uzuri pesa...pendeza sana mdada Mwanamuziki matata kabisaaa Linah sanga ... kwa haraka haraka hapo unaweza jua sio mtanzania... hakika alivunja rekod ya kupendeza akiwa katika muonekano huo...  @officiallinah  == je, mdau wewe unaonaje??? Funguka hapa

Jux Aanza Kuachia Picha Kutoka Kwenye Video Yake Mpya ‘One More Night’ Aliyoshoot South.

Image
Baada ya  Vanessa Mdee  kuachia video ya  ‘Never Ever’  mwezi uliopita,  Jux  naye ameanza ku-tease wimbo wake mpya, ikiwa ni ishara kuwa muda si mrefu anaweza kuachia kazi nyingine baada ya  ‘Looking For You’ . Moja ya picha za video hiyo Kwa wiki mbili sasa  Jux  amekuwa aki-tease picha (screenshot) za video ya wimbo huo, huku akiweka hashtag  ‘ONE MORE NIGHT’  kuashiria ndio jina la wimbo. Kwenye picha hizo ameandika captions hizi: -Natamani tusingefanya I need #onemorenight -Nilionja sijashiba #onemorenight #africanboy#somethingbigcoming -Baby I need one more night #africanboy #onemorenight Video mpya ya  Jux  ilishutiwa kipindi kimoja na  ‘Never Ever’  ya  Vanessa . Mwanzoni mwa mwezi September  Jux  na  Vanessa walienda  Afrika Kusini  kushoot video hizo na director  Justin Campos , na kushare baadhi ya picha za behind the Scene. BTS: Director Justin Cam...

ALI KIBA AONGEA KUHUSU YEYE NA KIDOTI

Image
Tangu wiki iliyopita kulikuwa na habari kuhusu ujauzito wa Jokate na Ali kiba akitajwa kama baba kijacho.baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kuhusu hilo.hatimaye amesema haya `sitaki kuzungumzia maisha yangu ya mapenzi na sio kweli k nategemea kupata mtoto na jokate` Ali kiba alisema hayo katika mahojiano na kituo kimoja cha habari nchini TANZANIA

Mshahara wa Mbunge ni Milioni 3.8 Kwa Mwezi, Posho ya Ubunge ni..

Image
Kwa mujibu wa Mh Zitto Kabwe: "Mshahara wa mbunge ni milioni 3.8 kwa mwezi, Posho ya Ubunge ni milioni 8 kwa mwezi, Posho ya kujikimu kwa siku ni laki 120,000 kwa siku, kukaa kikao cha bungeni posho ni shilingi laki 200,000 Kwa siku, pia bado bado kuna fedha kwaajili ya mfuko wa jimbo ambayo ni milioni 46 lakini hii hutegemeana na jimbo lenyewe na mbali na hapo kuna posho ya jimbo". Nini maoni yako hapo? Chanzo: East Africa Television (EATV)

Mchakato wa Kuanzisha Mahakama ya MAFISADI Waanza

Image
Utekelezaji wa ahadi za Rais John Magufuli unazidi kushika kasi baada ya kuanza kwa mchakato wa kuanzisha mahakama maalumu ya kuwashughulikia mafisadi. Jaji Kiongozi, Shaban Lila alisema jana kuwa tayari wadau mbalimbali wa haki jinai wameanza kukutana kuangalia namna ya kuanzisha mahakama hiyo kama sehemu ya utekejezaji wa ahadi ya Rais. Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya kushughulikia mashauri nyeti ya jinai kwa majaji 12 wa Mahakama Kuu ya Tanzania, alisema juzi walikuwa na mazungumzo na Wizara ya Katiba na Sheria kuangalia mfumo wa uendeshaji wa mahakama hiyo. “Tunaangalia tuianzishe kama mahakama huru au ifanywe ndani ya muundo wetu wa mahakama kwa kuipa kipaumbele maalumu. Lakini tunafikiria zaidi kama ingekuwa ni kitengo maalumu ndani ya Mahakama Kuu kitakachokuwa kikishughulikia mafisadi,” alisema Jaji Lila. Hata hivyo, Jaji Lila hakutaja muda maalumu utakaotumika kumaliza mchakato wa kuanzisha mahakama hiyo, huku akisema unahu...

Wabunge Waula Wachuya...Bunge Limekataa Kuongeza Dau Kwenye Hela ya Kununua Magari 'Mashangingi'

Image
hapa kazi tu,hatutaki mchezo na pesa za umma Msemaji wa Bunge amesema kuwa hawajapata malalamiko rasmi kutoka kwa wabunge kuwa wanahitaji kuongezea fedha hizo zifikie milioni 130 kutokana na kupanda kwa thamani ya dola ya Marekani. Mbunge Ezekiel Maige amesema kuwa afadhali Serikali iwanunulie magari kabisa kuliko kuwapa fedha Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF Abdallah Mtolea amesema wapewe fedha wakanunue wenyewe, pia amedai kuwa bei ya gari Land Cruiser(Mkonge) ambayo wabunge wanatakiwa kununua gharama yake sokoni ni milioni 130 Awali baadhi ya wabunge walidai kuwa wapewe milioni 130 kutokana na kupanda kwa bei ya magari wanayotakiwa kununua. Wabunge wa Bunge la 10 walipewa milioni 90 za kununua gari.

CHADEMA Yashinda Kesi......Mahakama Yatoa Kibali Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo Kuagwa na Kuzikwa

Image
Taarifa kutoka Mahakama kuu kanda ya Mwanza zinaarifu kuwa Familia ya Alphonce Mawazo na Chadema wameshinda kesi dhidi ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mwenyekiti huyo  wa Chadema Geita asiagwe  jijini Mwanza baada ya kuuawa kinyama kwa kukatwa mapanga  Amri ya Jeshi la polisi kuwa Mawazo asiagwe Mwanza kwa kuwa kuna hofu ya kipindupindu imetupiliwa mbali na Mahakama hiyo.  Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Lameck Mlacha imetoa ruhusa mwili wa Alphonce Mawazo kuagwa jijini Mwanza na imeagiza Jeshi la Polisi kutoa Ulinzi siku hiyo lakini Ulinzi huo usivuke mipaka. Sehemu ya hukumu ya kesi hiyo inasema "Kazi ya Polisi ni kulinda raia na si kuzuia mazishi.."

Mama Diamond Ambana Diamond Kuhusu Uhalali wa Mtoto Latiffah Katika Familia Yao..Mengi Yasemwa Mtaan

Image
Mama wa staa wa muziki Bongo, Sanura Kassim ‘Sandra’.SINEMA limeanza! Sanura Kassim ‘Sandra’ ni mama mzazi wa ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivi karibuni anadaiwa kuingia katika figisufigisu na mwanaye huyo kwa kumuhoji kama kweli Latiffah ‘Tiffah’ ni damu yake kwa kumzaa na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Amani limenyetishiwa. Akizungumza na mwandishi wetu Jumatatu ya wiki hii, mmoja wa wanandugu wa Diamond alisema ishu hiyo ilijiri hivi karibuni nyumbani kwa Diamond, Madale jijini Dar ambapo mama na mwana hao walikuwa katika mazungumzo ya kawaida. Ndipo, mama Diamond alipojikuta akiponyokwa na sentensi hiyo ya kuhoji uhalali wa Tiffah kuwa mtoto wa Diamond kauli ambayo awali ilichukuliwa kama utani wa bibi na mjukuu! ‘Kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.‘Yuda’ huyo wa Diamond, alizidi kusema kuwa, mama huyo alijikuta akimtaka Diamond aachane na wazo la kumhesabu Tiffah kama mwanaye kwani hafanani naye hata kidogo na kwamba ameuziwa mbuzi kwenye...

Lulu Awaogopa Wachawi Kumtaja Aliye Mtundika Ujauzito Wake MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa anaogopa wachawi kumtaja mhusika wa mimba aliyonayo. Lulu alifunguka hayo juzikati wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua mhusika wa mzigo alionao ndipo msanii huyo aliposema aachwe kwanza maana wachawi ni wengi.“Mh! Naomba mniache kwanza maana mjini hapa wachawi ni wengi, mambo yakiwa freshi kila mmoja atamjua,” alisema Lulu.

Image
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa anaogopa wachawi kumtaja mhusika wa mimba aliyonayo. Lulu alifunguka hayo juzikati wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua mhusika wa mzigo alionao ndipo msanii huyo aliposema aachwe kwanza maana wachawi ni wengi.“Mh! Naomba mniache kwanza maana mjini hapa wachawi ni wengi, mambo yakiwa freshi kila mmoja atamjua,” alisema Lulu.    MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa anaogopa wachawi kumtaja mhusika wa mimba aliyonayo. Lulu alifunguka hayo juzikati wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua mhusika wa mzigo alionao ndipo msanii huyo aliposema aachwe kwanza maana wachawi ni wengi.“Mh! Naomba mniache kwanza maana mjini hapa wachawi ni wengi, mambo yakiwa freshi kila mmoja atamjua,” alisema Lulu.   

Picha: HAMISA Mobeto Ajifungua Mtoto wa Kike, MIMBA yake ilikuwa SIRI Kubwa, Azaa na Mtangazaji Maarufu

Image
Modo maarufu na muigizaji chipukizi nchini, hamisa mobeto amejifungua mtoto wa kike. Staa huyo anayechipukia amejifungua ivi karibuni na kuwashangaza wengi kwani mimba hiyo ilikuwa na usiri mkubwa tofauti wafanyavyo mastaa wengine (zari ), Mobeto Amezaa mtangazaji maarufu Majizo ambae ni mkurugenzi wa EFM Hongera sana, duuh!! Ila hii mimba wambea wengi walikuwa hawajaipata, khaa!! Utatuua kwa presha aisehh loh, haya sasa nawapa assignment wambea wenzangu kumtambua au kumtaja baba mtoto wa hamisa

Loveness LOVE a.k.a Diva wa CLOUDS FM Abadili Jina, Sasa Anaitwa....

Image
Diva sio Loveness tena kuanzia sasa! Mtangazaji huyo wa Clouds FM amebadilisha jina lake mahakamani na kuwa ‘Diva Gissele D. Malinzi’ Diva ameaimbia Bongo5 kuwa kuanzia Jumatatu ijayo atabadilisha kila kitu kilichokuwa na jina lake la zamani ‘Loveness’ baada ya kula kiapo mahakamani cha kubadilisha jina. Kwenye kiapo hicho, Diva amedai ameamua kubadilisha jina hilo kwa sababu za kikazi kwakuwa amekuwa akitumia jina ‘Diva’ kwa kipindi kirefu sasa. “Professional purpose plus hayo ni majina yangu I so wanted ever since nakuwa, so amma grown up in my 20s, living in my own world, it’s Diva World I just live in it,” Diva ameiambia Bongo5 kuhusiana na sababu za kubadilisha jina. “ It’s Official I go by the name Diva Gissele Love ongeza surname mbele then we good to go. No More Loveness #abandoned and this deed already registered .. Thanks to My Lawyer Herry Munisi from Crest Attorneys . United Republic of Tanzania #ChangeOfName ,” ameandika kwenye Inst...

Waimbaji Walio Potea Katika Anga za Bongo Flava Marlaw na Besta Wapata Mtoto wa Pili..

Image
raha ya ndoa watoto Congrats Mr and Mrs Marlaw...... We Miss you Both Thooo.....

Ukweli Kuhusu Kupotea Kwa Shilingi MIA TANO ya Sarafu..Wajanja wa Mjini Watumia Kutengeneza CHENI..

Image
Ndani ya wiki moja nimekutana na watu watatu wakitafuta sh.500/= ya sarafu kwa sh.2500/= kwa sarafu moja ya mia 5, mwanzoni nilipuuzia lakini baada ya kutulia na kufanya utafiti nimegundua kwanza hii sarafu imekuwa adimu na inatafutwa kwa udi na uvumba  Pili ni kwamba wale wapenzi wa SILVER sasa unaweza kupata cheni halisi ya silver kwa bei poa kabisa ! sababu ni kwamba zile sarafu za mia tano ndio zinayeyushwa na kutengeneza vidani siku hizi Hii ni KASHFA nyingine kubwa kuhusiana na pesa yetu na mamlaka zinazohusika ziko kimya kuhusu hili lakini hii ndio hali halisi inayoendelea mitaani TUGUTUKE

Ang'atwa na Nyoka Akizini na Mke wa Mtu Kichakani

Image
Kijana mmoja shija kasamwa mwenye umri wa miaka 28,leo mchana amejikuta akipata masahibu ambayo iwapo atapona kamwe hatayasahau kabisa ktk maisha yake. Kijana huyo mkazi wa mkoa wa Shinyanga ktk kijiji cha Chela ameng'atwa na nyoka mwenye sumu kali akiwa msituni akivunja amri ya sita na mke wa mtu. Inasemekana ndio ilikuwa tabia yake kufanya uchafu huo na mwanamke huyo asiye mwaminifu ktk ndoa yake. Sasa leo kama kawaida yao walijirusha msituni,wakiwa huko kabla hawajaanza kufanya mapenzi walisikia sauti za watu wakija upande waliokuwepo ndipo wakaamua kuingia kichakani kwa hofu ya kuonekana,ndani ya kile kichaka kikubwa kilichokuwa kimefungasha miti mingi kiasi kwamba haikuwa rahisi kuonekana kwao,ndipo wakaamua kufanya uchafu wao eneo hilo ndipo wakiwa bado wanaendelea na starehe ilihali yule kijana akiwa kashusha suruali yake na makalio yake kubaki wazi alishtuka ghafla kang'atwa na nyoka huyo anayesadikiwa kuwa ni aina ya cobra,kelele za ...