;Biashara ya Maduka ya Dawa Baridi Muhimbili Yavurugwa
BIASHARA ya maduka ya dawa baridi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeingia shubiri, huku maduka mengine katika hospitali za Serikali yakitakiwa kuwa tayari baada ya agizo la Rais John Magufuli, kuanza kutekelezwa. Dk Magufuli alipoingia madarakani tu, moja ya maagizo yake alitaka Bohari ya Dawa (MSD) kufungua maduka ya dawa za Serikali kwenye hospitali za rufaa na za kanda, ambapo kesho kutwa Jumatatu duka hilo litaanza kufanya kazi Muhimbili na bei za dawa zitakuwa chini ya bei ya soko. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laureane Bwanakunu, amesema kufunguliwa kwa duka hilo kutaenda sambamba na kufunguliwa na duka lingine katika Hospitali ya Kanda ya Mbeya na baadaye kwenye hospitali zingine za rufaa na kanda na yatatoa huduma mpaka kwa wanaotumia utaratibu wa bima ya afya. Kwa mujibu wa Bwanakunu, pia MSD imeanza kuweka nembo ya Serikali kwenye vidonge na hadi sasa ina vidonge 45 ambavyo vimewekewa nembo ya GOT, ili ...