Posts

Showing posts from February 2, 2016

Hii sasa ni vita Zari, wema wapambana

Image
Wema Isaac Sepetu. DAR ES SALAAM: Hii sasa ni vita! Mpambano mkali umeibuka kwa mara nyingine kati ya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu na nyota wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Uganda, The Boss Lady’ ambaye pia ni mzazi mwenzake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Mapambano hayo yameanzia kwenye mitandao ya kijamii kisha kuhamia mitaani kwa timu zao ambapo baadhi ya watu wanasema kuna kitu zaidi katika chuki ya Zari kwa Wema. KUTOKA MTANDAONI Ni Zari ambapo inadaiwa, mapema wiki hii alitupia kwenye akaunti yake ya Instagram maneno yaliyotafsiriwa ni kejeli kwa Wema. Aliandika: Fake car (gari magumashi), fake house (nyumba magumashi), fake men (wanaume magumashi). Zari Hasan The Boss Lady’. Kisha akatupia ujumbe akijifanya anawasiliana na wifi yake, yaani dada wa Diamond aitwaye Esma Platnumz akimuuliza: Umelipa Tanesco? Wema aliwahi kudaiwa kuchezea mita ya Luku ya Shirika la Umeme (Tanesco) hivyo kusababisha deni la shilingi mi...

OFM yanusa jipu kivuko …

Image
DAR ES SALAAM: Kikosi Maalum cha Global Publishers cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ limenusa jipu katika Kivuko cha Kigamboni, Dar, jinsi baadhi ya abiria wa vivuko wanavyozamia kwenye ‘pantoni’ bila kulipa nauli, jambo linalotajwa kuikosesha serikali mapato. Dawati la OFM lilipokea malalamiko kutoka kwa raia wema, wakieleza jinsi ofisi za kivuko, upande wa Kigamboni zilivyo na mianya mingi ya watu kuingia bila kupitia getini na kupanda kwenye kivuko bila kulipa nauli, hali inayopoteza mapato ya serikali lakini pia kuhatarisha usalama wa abiria. “Kuna njia watu wanapita bila kuwa na tiketi, hawalipi nauli ya shilingi 200 wanayopaswa kulipa na pia kama mtu ana lengo baya, anaweza kuingia na silaha kama bunduki au bomu kwenye hivi vivuko viwili vya Mv Kigamboni na Mv Magogoni, akiamua kuwadhuru abiria hakuna kipingamizi, nyie fuatilieni mtaujua ukweli,” kilisema chanzo chetu. Baada ya kupata habari hizo, waandishi wetu walifunga safari mpaka Kivukoni na kujionea utar...

Range la Wema layeyuka

Image
   Staa wa muvi za Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu (kushoto) akiwa na gari yake gari aina ya Range Rover Evogue siku ya kuzaliwa kwake. DAR ES SALAAM: Staa wa muvi za Bongo na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ambaye hivi karibuni akisherehekea bathidei yake (siku ya kuzaliwa) alijitapa kujinunulia gari aina ya Range Rover Evogue kwa shilingi milioni 200, sasa inadaiwa kuwa, gari hilo halimiliki tena. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika kilichopo karibu na staa huyo, licha ya mwanadada huyo kujitapa kila kukicha kwa kumiliki mkoko huo ambao mara kadhaa kumekuwa na madai ya kwamba alihongwa, kwa sasa hayupo nalo tena na eti imebaki stori tu. Muonekano wa nyuma wa Range Rover Evogue hiyo. “Niwapashe wadaku, lile gari la bi shosti Wema alilojigamba kulinunua kwa jasho lake kwa shilingi milioni mia mbili, sasa hivi wala hayupo nalo. Alilipeleka gereji kufanyiwa matengenezo kisha akalipeleka yadi maeneo ya Kijitonyama kwa ajili ya kulipig...

Kwa hali hii Nchi inaliwa!

Image
Makongoro oging’, AMANI DAR ES SALAAM: Da! Wakati Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ akiendelea kutumbua majipu kwa vigogo mbalimbali serikalini, hasa wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Amani limenasa vigogo wengine wanne wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao wamejenga mahekalu ya mabilioni ya shilingi huku wakiishi maisha ya juu kama ‘miungu watu’, kweli nchi inaliwa! Awali, mahekalu mengine yaliyosemekana kuwa ni ya vigogo wa mamlaka hiyo, yalinaswa na kutolewa kwenye gazeti hili. CHANZO CHAZUNGUMZA NA AMANI Mapema wiki hii, chanzo chetu cha habari kilifika kwenye ofisi za gazeti hili na kuonana na wahariri wa Global Publishers kulalamikia maisha ya baadhi ya vigogo wa TRA kwamba ni ya anasa sana wakiwa wanaishi kwenye mahekalu (majumba) ya kifahari huku Watanzania walio wengi wanaishi kwa mlo mmoja tena kulala kwa kubanana. MSIKIE MWENYEWE “Jamani ndugu zangu, lengo la mimi kuja hapa ni kutaka kuwaambia kwamba, kuna vigogo wa TRA wanaishi Mbezi Beach. Wamejenga majumba ya kifa...

‘Msukule’ nyumbani kwa tajiri aibua mazito

Image
  Juhudi za kumtoa shimoni zikiendelea. Mayasa mariwata, AMANI DAR ES SALAAM: YULE mwanadada aliyekutwa kwenye shimo la majitaka ambalo halijaanza kutumika nyumbani kwa mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina moja la Mtei na kudhaniwa na watu kuwa labda ni msukule, Upa ameibua mazito. Kwa mujibu wa chanzo kutoka Jeshi la Polisi Kinondoni, mdada huyo ametoweka katika mazingira ya kutatanisha akiwa kwenye Kituo cha Polisi Mbezi jijini Dar tayari kwa kumpeleka hospitali. “Jamani mna habari yule dada aliyekutwa shimoni mwa mfanyabaioshara Mtei kule Kibamba, amepotea katika mazingira ya kutatanisha? Nimewaambia nyie maana nimeona leo (juzi Jumanne), mmeandika kwenye Gazeti la Uwazi,” alisema afande mmoja. Gazeti hili lilianza kufuatilia undani wa habari hiyo ambapo, vyanzo vya uhakika vinasema kuwa, ni kweli mwanamke huyo (mwenye watoto wawili) alitoweka kimaajabu. Baada ya kutolewa shimoni. Akizungumza na kituo kimoja cha redio cha jijini Dar, Jumatatu iliyo...

Bi Mwenda: Agoma Kufungukia Uchawi, Mme na Watoto

Image
 Mwenda. Katika kolamu hii tunayowaletea wasanii mbalimbali wa filamu kila wiki, leo tunaye nguli wa filamu Bongo, Fatuma Makongoro ‘Bi Chau’ ambaye pia aliwahi kutamba katika Kundi la Kaole lililokuwa na ‘vichwa vikali’ kama vile marehemu Steven Kanumba, Ray, Muhogo Mchungu, Kipemba, Dk. Cheni, Mtunisi, Frank, Nina, Nana, Norah, Kibakuli, Nyamayao, Max, Zembwela, Bambo, Kingwendu, Swebe, Zawadi na wengine wengi. Bi Mwenda amefunguka mengi kuhusiana na maisha yake kama alivyoulizwa na wasomaji wetu.Msomaji: Una muda gani tangu uanze sanaa na imekunufaisha vipi? Bi Mwenda: Nimeanza sanaa ya uigizaji mwaka 1998 na kusema kweli imeninufaisha sana, nimesomesha na pia nimejenga Musoma. Msomaji: Mara nyingi huwa nakuona kwenye usafiri wa daladala tofauti na wasanii wakubwa wengine ambao hupendelea kuwa na usafiri wao na wengine kukodi usafiri binafsi, uhofii hadhi yako kushuka? Bi Mwenda: Nihofie nini kwa mfano! Napenda kupanda daladala sababu hao wanaopanda ni binadamu kama m...