KIMENUKA..Miss Tanzania Atajwa Ufisadi wa Sh1.3 Trilioni
Aliyekuwa ofisa mwandamizi wa benki ya Stanbic tawi la Tanzania, Shose Sinare amehusishwa na mipango ya kifisadi ambayo imeisababishia Serikali ya Tanzania hasara ya Sh1.3 trilioni kati ya mwaka 2012 na 2013. Taarifa ambazo gazeti hili limepata kutoka Uingereza na hapa nchini, mwanadada huyo ambaye alikuwa mrembo wa Tanzania mwaka 1996, alishirikiana na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bashir Awale. Sinare hakupatikana kufafanua suala hilo ilhali Awale alifukuzwa nchini hivi karibuni. Alipoulizwa jana kuhusu tuhuma hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hosea alisema anatambua suala hilo, linafuatiliwa na taasisi yake na hakutaka kutoa maelezo zaidi. Taarifa kwamba Serikali imetumbukia katika kashfa nyingine kubwa ya ufisadi zimebainika baada Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Ufisadi ya Uingereza (SFO) kuwasilisha mahakamani ushahidi wake kwamba kiasi cha Sh1.3 trilioni kilipotea wakati wa uuzwaji wa hati fungani za Serikali kwa benki ya Stan...