Mke wa Lowassa Mama Regina Lowassa MGOGORO wa vyama viwili vya siasa CUF na CHADEMA ambavyo vinaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), katika Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, juzi ulichukua sura mpya. Hali hiyo inatokana na mgombea mmoja wa ubunge wa jimbo hilo kupitia CUF, Martine Makondo na wafuasi wake, kuvamia uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa CHADEMA, Martine Magire ambapo mgeni alikuwa Mama Regina Lowassa (mke wa Edward Lowassa). Mama Lowassa alishindwa kuzindua kampeni hizo kutokana na vurugu kubwa zilizotokea. Awali mkutano ulikuwa ufanyike kwenye Uwanja wa Michezo uliopo katika Sekondari ya Lagangabilili. Dalili za vurugu zilianza kuonekana mapema baada ya wafuasi wa CHADEMA kudai kuwa, mgombea wa CUF alikuwa amekwenda kwenye mkutano huo na kundi la vijana ili kuvuruga mkutano. Baada ya Mama Lowassa kuwasili eneo la mkutano akiwa na Naibu Katibu Mkuu Baraza la Wanawake wa CHADEMA Taifa (BAWACHA),Kunti Yusuph, mgombea wa CUF aliwasili ene...