Posts

Showing posts from September 16, 2015

MKE WA SLAA AJIBU MAPIGO YA GWAJIMA

Image
MKE wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Dk. Willibrod Slaa, Josephine Mushumbusi,  ambaye amekuwa akitupiwa tuhuma nyingi za kumponza na kumsababishia aibu mume wake amesema kuwa hajaona jambo lolote lenye maudhui ya kujibu tuhuma zinazoelekezwa dhidi yake. Kauli hiyo ya Mushumbusi imekuja siku chache baada ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye Dk. Slaa alimtaja kama mshenga wa tukio la Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kujiunga na Chadema, kudai ana ushahidi unaoonyesha kuwa mama huyo ndiye chanzo cha mume wake kuacha siasa. Mushumbusi ambaye yuko nje ya nchi, alitoa msimamo huo katikati ya wiki hii wakati akiwasiliana na MTANZANIA Jumamosi kwa njia ya barua pepe. Amejipambanua kwa kusema kwamba mafanikio yake yataonekana muda si mrefu hivyo kwa sasa amefunga mikono. “You will see ...

Maneno mengine ya T B Joshua mwaka mmoja baada ya Jengo la Kanisa lake kuanguka Umepita mwaka mmoja sasahivi toka litokee tukio la kuanguka kwa Jengo la Kanisa la Synagogue Church of All Nations Nigeria ambalo linaongozwa na Mchungaji T B Joshua… kuna watu wengi walifariki katika tukio hilo na ilikuwa stori ambayo iligusa watu wengi kwa sababu ya umaarufu wa Mchungaji huyo nje ya mipaka ya Nigeria. T B Joshua ameandika ujumbe unaogusa kumbukumbu ya tukio hilo, kwenye alichokisema kuna haya maneno pia >>> ‘Ni muhimu kukumbuka kwamba sisi ni Familia ya MUNGU, wakati mwingine kwenye mazingira kama haya tunatakiwa kumuachia MUNGU… Tunatakiwa kuamini kwamba vifo vya ndugu zetu ilikuwa ni mapenzi ya MUNGU, na haikuwezekana kupingana nao‘- T B Joshua. 3 Ajali ya kuanguka kwa Jengo la Kanisa hilo ilitokea September 12 2014, ambapo watu 115 walifariki na 84 kati yao walikuwa Raia wa South Africa.

Image
Umepita mwaka mmoja sasahivi toka litokee tukio la kuanguka kwa Jengo la Kanisa la Synagogue Church of All Nations  Nigeria ambalo linaongozwa na Mchungaji T B Joshua … kuna watu wengi walifariki katika tukio hilo na ilikuwa stori ambayo iligusa watu wengi kwa sababu ya umaarufu wa Mchungaji huyo nje ya mipaka ya Nigeria. T B Joshua ameandika ujumbe unaogusa kumbukumbu ya tukio hilo, kwenye alichokisema kuna haya maneno pia >>> ‘ Ni muhimu kukumbuka kwamba sisi ni Familia ya MUNGU, wakati mwingine kwenye mazingira kama haya tunatakiwa kumuachia MUNGU… Tunatakiwa kuamini kwamba vifo vya ndugu zetu ilikuwa ni mapenzi ya MUNGU, na haikuwezekana kupingana nao ‘- T B Joshua . Ajali ya kuanguka kwa Jengo la Kanisa hilo ilitokea September 12 2014, ambapo watu 115 walifariki na 84 kati yao walikuwa Raia wa South Africa.

Lil Wayne na Christina Millian waachana..!? Sababu? Ninayo yote hapa

Image
Baada ya kuachana na mchumba wake miaka miwili iliyopita mwimbaji wa R&B Christina Millian alianza kuonekana sana na rapper Lil Wayne baada ya kujiunga na lebo ya msanii huyo, muda mfupi badaae wawili hao wakaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mpaka sasa wana zaidi ya mwaka mmoja pamoja. Christina Millian na Lil Wayne. Lakini leo headlines za wawili hawa ni tofauti kidogo… wapenzi hao wamethibitisha kuwa wameachana toka mwezi uliyopita lakni waliamua kukaa kimya kwanza na kuweka baadhi ya mambo yao sawa kabla kutangaza kwa watu kuwa uhusiano wao wa kimapenzi umeisha. Msemaji wa karibu wa watu hao anasema sababu kubwa iliyopelekea kuachana kwao zinatokana na ratiba za wawili hao kubana sana. >>> “Wanaachana sio kwamba wanapenda ila ratiba zao zinawabana sana, wanakosa muda wa kuonana na kuwa pamoja, Lil Wayne anafanya sana tour za wasanii wake na za kwake pia  na pia anaifanyia kazi...

Kisa Pombe; Johari Azima, Akombwa Kila Kitu

Image
Kisa pombe! Mwigizaji wa kitambo Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ anadaiwa kupiga mitungi hadi akazima kisha kukombwa mkoba uliokuwa na kila kitu zikiwemo fedha taslimu Sh. 285,000/= na simu ya ‘tachi’ ya bei mbaya. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita kwa njia ya simu akiwa mkoani Tabora ambako Johari na baadhi ya mastaa wengine wapo kwa kazi maalum, mmoja wa wasanii hao alitonya kuwa tukio hilo lilijiri Alhamisi usiku, wakati wakiwa wanagida pombe, jambo lililozua taharuki kwake na wenzake. Mtonyaji huyo alifunguka kuwa, wakiwa wanaendelea kunywa, Johari alifika wakati akazima ambapo walikuja watu waliojiita mashabiki wake, wakawa wanamvizia hivyo alipozinduka akaenda maliwatoni na kuacha mkoba wake, aliporudi ndipo akagundua kuwa mkoba wake haukuwepo, hali iliyomfanya aangue kilio cha uchungu. Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, mwandishi wetu alimtafuta msanii rafiki wa damu na Johari (jina tunalo) ambapo aliombwa kumpa simu Johari ili kuzungumza naye ...

Je wajua ngoya ya Navy Kenzo GAME ni copy?, Pia Weusi wamekataa kampeni? mapya ya Bonge la nyau

Image
Kwenye zile headlines za burudani leo 255  Producer wa The Industry Studios aliyetengeneza ngoma ya ‘GAME’ ya Navy Kenzo Feat.Vanessa Mdee amezungumzia beat ya ngoma hiyo kufananishwa na ngoma ya Girlie ‘O’ ya Patoranking feat.Tiwa Savage , amesema Watanzania wengi hawaamini wala hawapendi kuona wenzao wanafanya vizuri, lakini wanapaswa kujua wanafanya nini, anasema ana mazungumzo mazuri sana na Patoranking na kama kuna tatizo angemwambia. Lameck Philipo au Bonge la nyau ametangaza a.k.a. nyingine ya jina lake kuwa ni Nyauloso, amesema wengine walikuwa hawalipendi wakisema jina ni baya lakini sasa hivi wanalipenda jina la ‘Nyauloso ‘..anasema awali kuna msichana alimpa jina la ‘Big Cat’ na kulibadilisha kuwa ‘Bonge la Nyau’ na Nyauloso alipewa na x-girlfriend wake. Bonge la Nyau Joh Makini amezungumza na kusema walikua na maisha kabla ya kampeni lakini hawezi kusema kama walishindwa kufika bei na watu wa vyama kuhusu kufanya kampeni, anasema wanaepuka ku...

Mama Diamondi atoka mbio kisa Zari soma hapa ujue kisa

Image
Mama wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kasim. KWELI maisha si popote! Msemo huu wenye kinyume na ule usemao maisha ni popote umedhihirika baada ya hivi karibuni mapaparazi wetu kutonywa kuwa, mama wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kasim amekuwa akimkimbia mkaza mwanaye, Zarinah Hassan ‘mama Tiffah’ ndani na kwenda kukaa nje kutokana na Zari kujikita sana kwenye mitandao ya kijamii hivyo kutokuwa na mawasiliano. Zarinah Hassan ‘mama Tiffah’. “Mnajua mama Diamond hana neno. Anaweza kukaa na Zari wakaongea, tatizo Zari. Muda mwingi yupo kwenye Instagram, mara WhatsApp, ukiangalia mama yeye na mambo hayo si sana. Anajikuta yuko mwenyewe tu. “Ndiyo maana inafika wakati inabidi mwanamke huyo atoke ndani na kwenda kushinda nje. Zari mara nyingi yeye yupo na simu kwenye eneo la bwawa la kuogelea,” kilisema chanzo. Mama wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kasim. UZUNGU KWA SANA Chanzo kiliendelea kueleza kuwa, maisha ya mama ...

MVUTANO..Mtoto wa Diamond kuwagombanisha na Zari

Image
Ndivyo unavyoweza kusema baada mastaa wapendanao, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kujikuta wakipishana kauli kutokana na mvutano wa kibiashara unaohusu Sherehe ya Arobaini ya mtoto wao mchanga, Latiffah Nasibu ‘Tiffah’ ambaye amedhaminiwa Sh. Mil. 40 na makampuni mbalimbali yanayojishughulisha na bidhaa za watoto, Ijumaa Wikienda lina ‘full’ stori. Mtoto wa Diamond na Zari, Latiffah Nasibu ‘Tiffah'. TUJIUNGE NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo, mvutano wa wawili hao umeanzia katika suala la kujadili eneo la kufanyia sherehe hiyo inayotarajiwa kufanyika Septemba 20, mwaka huu ambapo Diamond anataka sherehe ifanyikie katika ukumbi mkubwa kama yalivyopendekeza makampuni hayo yanayogombea ubalozi na kudhamini tukio hilo lakini Zari anataka ifanyike nyumbani. “Diamond amefuata biashara zaidi. Makampuni yanayodhamini shughuli hiyo yamemwambia ili azma yao ya kutangaza bidhaa zao itimie, inabidi wafanyie kwenye ukumbi mkubwa ili watu ...

Breaking News: Mtangazaji wa Clouds FM DJ Fetty Atangaza Kuacha Kazi Clouds

Image
September 15 2015 Show ya XXL inaandika Historia nyingine tofauti ambapo DJ Fetty ametangaza kuacha kazi ya Utangazaji na kuingiza nguvu yake zaidi kwenye masuala ya Biashara… wakati Fetty anatangaza hivyo, presenter mwingine pia Kened the Remedy ameungana na Timu ya XXL kwa mara ya kwanza.

Baada ya kununua Prado, Nay wamitego aasema ‘kinachofuata ni Range Rover’

Image
Nay wa Mitego amesema akimaliza ujenzi wa nyumba yake mpya ya kifahari iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam, atanunua gari aina ya Range Rover. Nay ambaye amenunua gari mpya, Prado Land Cruiser hivi karibuni, ameiambia Bongo5 kuwa lengo lake ni kumiliki Range. “Bado sijapata gari ninayoihitaji, mpango wangu ni Range nikimaliza nyumba yangu ya Tabata,” alisema Nay. “Hii Prado ni mpya lakini ina kazi maalum. Hii ni kwaajili shows za mikoani. Nimenunua milioni 60, ni mpya kabisa ndio maana unaona hata namba haina ila ikikamilika kila kitu itakuwa barabarani soon.

Tundu Lissu Ajibu Mapigo.......Asema Mwenye Richmond ni Rais Kikwete Mwenyewe

Image
Wednesday, September 16, 2015 Siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amtaje mhusika wa Richmond anayezunguka naye kwenye kampeni, Mbunge huyo wa Singida Mashariki ameibuka na kudai kuwa Rais huyo ndiye mhusika kwa kuwa ndiye mwenye mamlaka ya kuteua na kuwawajibisha mawaziri. Juzi, akiwa Kigoma, Rais Kikwete alieleza kumshangaa Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mtu huyo anazunguka naye kwenye mikutano ya kampeni na kumtaka amtaje la sivyo yeye (Rais), atamtaja. Akihutubia mkutano wa kumnadi mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, mwanasheria hiyo alianza kwa kusema: “Sasa ndugu zangu naomba leo nimjibu Kikwete na tumalizane na hii habari ya Richmond." Alisema mkuu huyo wa nchi ndiye mhusika kutokana na mamlaka yake na; “si ya huyu Lowassa anayedai natembea naye kwenye kampeni. Hapa kwenye mkono wangu nina taarifa ya mwaka 2008 ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Richmond,...

Balaah Diamond Platnumz apokea ushindi wa tuzo nyingine mbili…!!

Image
on September 16, 2015 Mwaka huu umekuwa mzuri sana kwa mtu wetu Diamond Platnumz kwani amekuwa wa kupokea na kutajwa kwenye tuzo nyingi sana kwa mwaka huu wa 2015 na siku chache zilizopita Diamond Platumz alitajwa kuwania tuzo nyingine tena za kimatatifa MTV EMA 2015 jijini Milan Italy . Headlines za Diamond Platnumz haziishii hapo, good news kwako mtu wangu msanii wetu wa Bongo Flava anazidi kuonyesha ubora wake kwenye nafasi mbalimbali za tuzo Africa … Diamond amepokea ushindi wa tuzo nyingine tena! African NAFCA Awards 2015 imemtaja Diamond kuwa Msanii wa mwaka anaependwa na wimbo wa ‘ Nana’ umetajwa kuwa Wimbo wa mwaka unaopendwa ! Kupita page yao ya Instagram   @africannafca walipost picha hizi za tuzo za Diamond Platnumz … 1.Diamond Platnumz favorite artist of the year.   I would love to say thank you to everybody who Voted for me on @africannafca Awards...am so grateful, i wouldn't have Made it without you...