Posts

Showing posts from November 20, 2015

MAGAIDI WALIJIFANYA WAHAMIAJI:UFARANSA

Image
Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls. Waziri mkuu wa Ufaransa,Manuel Valls, amesema kwamba watu wanaohusishwa na kundi la Islamic State ambao walitekeleza shambulizi mjini Paris wiki iliyopita,ambalo liligharimu uhai wa watu mia moja na ishirini na tisa,waliingia nchini humo kwa mgongo wa sakata la uhamiaji barani ulaya na kuzamia nchini Ufaransa bila kugundulika. Ameyasema hayo wakati alipokuwa anazungumza katika runinga ya taifa hilo na kwamba wahusika wengine wa ugaidi walikuwemo katika nchi za Ufaransa na Ubelgiji mapema. Waziri huyo aliongeza kuwa haikufahamika mara moja kwamba kulikuwa na makundi ya namna hiyo kwa ukubwa wake ,ama mshukiwa Salah Abdeslam, ambaye ndiye hasa kielelezo cha mwanamume anayesakwa zaidi kimataifa na haikujulikana kama alikuwa Ubelgiji ama Ufaransa.

LIPUMBA: MAGUFULI ANAKABILIWA NA HALI NGUMU YA BAJETI

Image
Profesa Ibrahim Lipumba. HATIMAYE aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF aliyejiuzulu uenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba ameibuka na kusema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli anakabiliwa na hali ngumu ya bajeti kwa kipindi kijacho cha miaka mitano. Akizungumza na wanahabari katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni jijini Dar leo, Lipumba amesema Rais Magufuli anakabiliwa na mambo kadhaa yakiwemo ya hali ngumu ya bajeti ya serikali kufuatia taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwezi Oktoba 2015 kuonesha kuwa, mwaka wa fedha 2014/2015 serikali ilipanga kukusanya mapato ya ndani ya shilingi bilioni 12,178 ikiwa sehemu kubwa ni makusanyo ya mapato ya Tanzania Revenue Authority (TRA). Aidha aliendelea kufafanua kuwa, serikali ilikusanya shilingi bilioni 10,507 mapato halisi ukilinganisha na bajeti kwa kiasi cha shilingi bilioni 1,671 sawa na 14% ya malengo ya bajeti. Akaongeza kuwa, halmashauri za wilaya, miji na maji...

MTANGAZAJI PRINCE BAINA KAMKURU AFARIKI DUNIA

Image
Share on google_plusone_shar Share on twitte Share  Prince Baina Kamkuru enzi za uhai wake. Mtangazaji wa zamani wa Radio Free Afria (RFA), Clouds FM na Star TV, Prince Baina Kamkuru amefariki dunia ghafla jana usiku akiwa jijini Dar es Salaam. Taarifa za awali kuhusu kifo cha marehemu Kamkuru zinaeleza kuwa alianguka ghafla wakati akifanya mazoezi ya viungo na alipokuwa akiwahishwa hospitali kwa matibabu alifariki dunia. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda mkoani Kagera kwa mazishi siku ya Jumapili na kwa sasa msiba upo Kigamboni jijini Dar. (rerst in peace )