JESHI LA POLISI SASA WANAMSAKA "DAUDI BALALI" NI YULE ALIYEWAHI KUWA GAVANA WA BENKI KUU BOT ...WAAHIDI KUMPAT
Jeshi la Polisi nchini linafanya uchunguzi kumbaini mmiliki wa ukurasa wa twitter unaoendeshwa na anayejiita Daudi Balali, aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake. Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba, aliyasema hayo wakati akizungumza na Nipashe ofisini kwake jana. Bulimba alisema kuwa taarifa za uwapo wa ukurasa huo wa twitter, wamekwishazipata na wanafanya uchunguzi wa kina kumkamata mhusika kisha kumfikisha kwenye vyombo vya sheria. “Tunazo taarifa juu ya ukurasa huo wenye wafuasi wengi kwa sasa na unaotumika kuwashambulia viongozi wa serikali na wa siasa hasa wale wanaogombea nafasi kubwa za utawala nchini, hivyo Jeshi la Polisi lipo kwenye uchunguzi ili kumbaini mtu huyo haraka iwezekanavyo,” alisisitiza Senso. Ukurasa huo ulioanza kutumika kabla ya Sheria ya Uhalifu wa Mtandaoni kuanza kutumika, una wafuasi zaidi ya 6,000 kwa sasa na umekuwa ukitumika kuwachafua wag...