Posts

Showing posts from November 28, 2015

PICHA ZA TUKIO ZA INSTAGRAM PARTY TANZANIA JIJINI DAR ES SALAAM ESCAPE ONE

Image
Freconic Ideaz gives you an Opportunity to Experience Instagram into real life. Join the fun to get Connected and Entertained. Tonight at Escape One - Mikocheni we will giving you the best of all times

Kasi Rais Magufuli Yamkumba Kamishna Mkuu wa TRA Afukuzwa Kazi Kwa Upotevu wa Makontena zaidi ya 349 Bandarini...

Image
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemsimamisha kazi kuanzia jana tarehe 27 Nov. 2015, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndugu Rished Bade kufuatia ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kasimu Majaliwa mapema jana asubuhi Bandarini jijini Dar es salaam.   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) kuhusu upotevu wa makontena zaidi ya 349 huku akiwa ameshika nyaraka yenye orodha ya makontena hayo. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akionesha nyaraka hiyo mbele ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano huo. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakwanza kushoto akifafanua jambo mbele ya wanahabari.

Sasa Tunakwenda Kushuhudia Tofauti ya UKAWA Kushika Dola na CCM Kurudi Madarakani

Image
Tutakachoshuhudia katika awamu hii ni kuibuliwa kwa madudu makubwa huku wakuu wa mashirika ya umma wakiwajibishwa kama mbuzi wa kafara lakini vigogo walioko kwenye system wakipeta au wakikamatwa wale dagaa tu. Inawezekana kabisa,hawa wakuu wa mashirika haya ya umma walikuwa wanafanya kazi tu ya kulinda maslahi ya wakubwa na huenda wao wakawajibishwa huku vigogo hawa wakiachwa jambo ambalo serikali ya UKAWA isingelifanya. Kumekuwepo na madai/tuhuma za vigogo kutumia majina ya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kuendesha biashara zao kitu ambacho sidhani kama serikali ya Magufuli itathubutu kukufanyia uchunguzi-UKAWA wangethubutu. Hivi biashara ya madawa ya kulevya, magogo,meno ya tembo na hata hii ya kupitisha makontena kiholela bandarini haina baraka za wakubwa?Magufuli ataweza kuwawajibishi vigogo hawa pindi wakibainika? Fukuafukua hii ya serikali ya Magufuli huenda ikawa "counter-productive" kwa CCM na serikali yake na jambo hili likiwa handled vibaya, huenda likafanya w...