CHADEMA Yashinda Kesi......Mahakama Yatoa Kibali Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo Kuagwa na Kuzikwa


Taarifa kutoka Mahakama kuu kanda ya Mwanza zinaarifu kuwa Familia ya Alphonce Mawazo na Chadema wameshinda kesi dhidi ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mwenyekiti huyo  wa Chadema Geita asiagwe  jijini Mwanza baada ya kuuawa kinyama kwa kukatwa mapanga 
Amri ya Jeshi la polisi kuwa Mawazo asiagwe Mwanza kwa kuwa kuna hofu ya kipindupindu imetupiliwa mbali na Mahakama hiyo. 
Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Lameck Mlacha imetoa ruhusa mwili wa Alphonce Mawazo kuagwa jijini Mwanza na imeagiza Jeshi la Polisi kutoa Ulinzi siku hiyo lakini Ulinzi huo usivuke mipaka.
Sehemu ya hukumu ya kesi hiyo inasema "Kazi ya Polisi ni kulinda raia na si kuzuia mazishi.."

Comments

Popular posts from this blog

Ang'atwa na Nyoka Akizini na Mke wa Mtu Kichakani

Kubenea Aibua Ufisadi wa Billion 1.2 Kupitia Ufuaji wa Majoho ya Madiwani

Tundu Lissu Ajibu Mapigo.......Asema Mwenye Richmond ni Rais Kikwete Mwenyewe