Posts

Showing posts from November 17, 2015

Robert Mugabe: Raila Odinga akikanyaga Zimbabwe nitamkamata na kumhasi

Image
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amemshambulia kwa maneno mwanasiasa mkongwe wa Kenya ambaye pia ni kiongozi wa chama cha CORDS huku akimpiga marufuku kukanyaga ardhi ya nchi hiyo. Akizungumza huko Marondela katika hafla iliyowahusisha wanajeshi walioshiriki katika vita mbalimbali, Mugabe alimtuhumu Raila kwa kutaka kumpindua kwenye nafasi yake kwa kuwapandikiza wapinzani nchini humo. Hivi ndivyo alivyosema: “Raila Odinga ni mwanasiasa muongo wa Kenya, mwanaume mnafiki ambaye yuko katika mkakati wa kuwapandikiza marafiki zake kuwa marais kwenye nchi zote za Afrika ili awe mwenyekiti mwenye nguvu kwenye Umoja wa Afrika (AU), siku moja watamuangusha kwenye sanduku la kura. “Angalia alichokifanya Nigeria, Tanzania, Ivory Coast na anataka kufanya hivyo pia Uganda kwa kumtumia rafiki yake Kiiza Besigye ambaye leo anapewa sifa na ushupavu ambao anapata kutokana tu na amri za Raila barani Afrika. “Hapa hatutamruhusu kuwageuza marafiki zake wa zamani Tendai Bi...