Mimba ya Jokate Yazua Balaa, Familia Yashtuka
Kwani kimenuka? Siku chache baada ya kubumburuka kwa habari ya kunasa mimba ikimhusisha ‘mtoto mzuri’ Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ huku mhusika mkuu akitajwa kuwa ni msanii nguli wa Bongo Fleva, Ali Kiba, ishu hiyo imezua balaa kufuatia familia ya mrembo huyo kushtushwa na hali hiyo, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa. TWENDE OYSTERBAY Mwishoni kwa wiki iliyopita, ‘kijumbe’ wa gazeti hili alitua getini nyumbani kwa akina Jokate, Oysterbay jijini Dar kwa lengo la kutaka kujua nini kinaendelea juu ya binti yao kunasa mimba nje ya ndoa ilihali familia hiyo inasifika kwa misingi bora na maadili ya kidini. Gazeti hili lilipotia timu nyumbani hapo, lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa wanafamilia hiyo aliyekuwa nje akifanya usafi ambaye bila simile ‘alifunua kinywa’ na kuweka hadharani mambo mazito. GAZETI LA IJUMAA LAIBUA MAMBO Kama anayeogopa jambo fulani, memba huyo wa familia ya Jokate alisema kuwa, mrembo huyo alikuwa akifanya siri kubwa juu ya ujauzito wa...