Posts

MAGAIDI WALIJIFANYA WAHAMIAJI:UFARANSA

Image
Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls. Waziri mkuu wa Ufaransa,Manuel Valls, amesema kwamba watu wanaohusishwa na kundi la Islamic State ambao walitekeleza shambulizi mjini Paris wiki iliyopita,ambalo liligharimu uhai wa watu mia moja na ishirini na tisa,waliingia nchini humo kwa mgongo wa sakata la uhamiaji barani ulaya na kuzamia nchini Ufaransa bila kugundulika. Ameyasema hayo wakati alipokuwa anazungumza katika runinga ya taifa hilo na kwamba wahusika wengine wa ugaidi walikuwemo katika nchi za Ufaransa na Ubelgiji mapema. Waziri huyo aliongeza kuwa haikufahamika mara moja kwamba kulikuwa na makundi ya namna hiyo kwa ukubwa wake ,ama mshukiwa Salah Abdeslam, ambaye ndiye hasa kielelezo cha mwanamume anayesakwa zaidi kimataifa na haikujulikana kama alikuwa Ubelgiji ama Ufaransa.

LIPUMBA: MAGUFULI ANAKABILIWA NA HALI NGUMU YA BAJETI

Image
Profesa Ibrahim Lipumba. HATIMAYE aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF aliyejiuzulu uenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba ameibuka na kusema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli anakabiliwa na hali ngumu ya bajeti kwa kipindi kijacho cha miaka mitano. Akizungumza na wanahabari katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni jijini Dar leo, Lipumba amesema Rais Magufuli anakabiliwa na mambo kadhaa yakiwemo ya hali ngumu ya bajeti ya serikali kufuatia taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwezi Oktoba 2015 kuonesha kuwa, mwaka wa fedha 2014/2015 serikali ilipanga kukusanya mapato ya ndani ya shilingi bilioni 12,178 ikiwa sehemu kubwa ni makusanyo ya mapato ya Tanzania Revenue Authority (TRA). Aidha aliendelea kufafanua kuwa, serikali ilikusanya shilingi bilioni 10,507 mapato halisi ukilinganisha na bajeti kwa kiasi cha shilingi bilioni 1,671 sawa na 14% ya malengo ya bajeti. Akaongeza kuwa, halmashauri za wilaya, miji na maji...

MTANGAZAJI PRINCE BAINA KAMKURU AFARIKI DUNIA

Image
Share on google_plusone_shar Share on twitte Share  Prince Baina Kamkuru enzi za uhai wake. Mtangazaji wa zamani wa Radio Free Afria (RFA), Clouds FM na Star TV, Prince Baina Kamkuru amefariki dunia ghafla jana usiku akiwa jijini Dar es Salaam. Taarifa za awali kuhusu kifo cha marehemu Kamkuru zinaeleza kuwa alianguka ghafla wakati akifanya mazoezi ya viungo na alipokuwa akiwahishwa hospitali kwa matibabu alifariki dunia. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda mkoani Kagera kwa mazishi siku ya Jumapili na kwa sasa msiba upo Kigamboni jijini Dar. (rerst in peace )

Robert Mugabe: Raila Odinga akikanyaga Zimbabwe nitamkamata na kumhasi

Image
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amemshambulia kwa maneno mwanasiasa mkongwe wa Kenya ambaye pia ni kiongozi wa chama cha CORDS huku akimpiga marufuku kukanyaga ardhi ya nchi hiyo. Akizungumza huko Marondela katika hafla iliyowahusisha wanajeshi walioshiriki katika vita mbalimbali, Mugabe alimtuhumu Raila kwa kutaka kumpindua kwenye nafasi yake kwa kuwapandikiza wapinzani nchini humo. Hivi ndivyo alivyosema: “Raila Odinga ni mwanasiasa muongo wa Kenya, mwanaume mnafiki ambaye yuko katika mkakati wa kuwapandikiza marafiki zake kuwa marais kwenye nchi zote za Afrika ili awe mwenyekiti mwenye nguvu kwenye Umoja wa Afrika (AU), siku moja watamuangusha kwenye sanduku la kura. “Angalia alichokifanya Nigeria, Tanzania, Ivory Coast na anataka kufanya hivyo pia Uganda kwa kumtumia rafiki yake Kiiza Besigye ambaye leo anapewa sifa na ushupavu ambao anapata kutokana tu na amri za Raila barani Afrika. “Hapa hatutamruhusu kuwageuza marafiki zake wa zamani Tendai Bi...

BREAKING NEWS MCHUNGAJI MTIKILA AFA KATIKA AJALI ....mtikila

Image
Mchungaji Mtikila Enzi za uhai wake Mwanasiasa maarufu nchini Tanzania mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia kwa ajali ya Gari leo Majira ya saa 10 alfajiri akitokea mkoani kwake Njombe katika kampeni .  Taarifa zilizothibitishwa na mgombea Ubunge jimbo la Iringa Mjini na mwenyekiti wa DP Mkoa Robart Kisinini wakati akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz amesema ni kweli mwenyekiti wake huyo Taifa amefariki dunia  , RPC Pwani amesema ni kweli kuna ajali imetokea eneo la Msolwa ameenda kwenye eneo la tukio na atatoa taarifa baadae ajali hiyo imetokea  eneo la Msolwa mkoani Pwani huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa taarifa zaidi ataitoa baada ya kurejea kutoka  eneo la tukio  

Baada ya kushinda Kesi ya UBAKAJI, flóra mbasha amapandisha Tena mumewe mahakamani Kwa Hili ..

Image
SIKU baada chache kushinda ya Kesi ya tuhuma za kubaka iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, mwimbaji wa muziki wa Injili, Emmanuel Mbasha anatarajiwa kupandishwa Tena katika korti hiyohiyo Kwa Madai mengine, Risasi Mchanganyiko iomlána habari Lina. Mwimbaji wa muziki wa Injili, Emmanuel Mbasha. Akizungumza na gazeti Hili hivi karibuni Kwa sharti la kutotajwa Jina, wa watu wa mmoja karibu na wanandoa Hao, alisema Flóra amefungua Kesi ya Madai ya talaka katika Mahakama ya Kisutu na kwamba muda si mrefu shauri HILO litaanza kusikilizwa. "Flóra ameenda mahakamani kudai talaka Yake, hiyo Kwa Kesi inatarajiwa kuanza kusikilizwa muda wowote kuanzia Sasa," alisema mtoa habari huyo.Baada ya hizo taarifa, mwandishi wetu alimtafuta Mbasha Kwa njia ya Mobile na kumuuliza Barr ya Madai hayo, ambapo alikiri na kudai anajiandaa kukabiliana na shitaka HILO. "Yeah, ni kweli Kaka, Flóra ameamua kwenda mahakamani kudai t...

Ali Kiba na Hasheem wagongana kumuoa Jokate! Mkasa upo ha

Image
m astaa katika category tofauti, Ali Saleh Kiba na Mtanzania anayecheza mpira wa kikapu nchini Marekani (NBA), Hasheem Thabit Manka, wanadaiwa kuchuana vikali kila mmoja akiwania kumuoa mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ huku mama mzazi wa mrembo huyo akitia ngumu, Risasi Jumamosi linaweza kuripoti. TAARIFA ZA AWALI Habari za awali, zilizovujishwa na mtoa taarifa wetu ambaye ni rafiki wa karibu na familia ya Jokate, juzi Jumatano zilieleza kwamba, kwa sasa kuna vita baridi kati ya Hasheem na Kiba kwa kila mmoja kutumia njia mbadala ili kuhakikisha anamuweka kibindoni mrembo huyo. MPASUKO NDANI YA FAMILIA “Lakini wakati hilo likiendelea, kuna taarifa kwamba kuna mpasuko kwenye familia ya Jojo (Kidoti). Inasemekana mama wa mrembo huyo anampa nafasi kubwa Hasheem. “Lakini kwa upande wake, Jokate amekuwa akimnadi Kiba, jambo linalozua mpasuko mkubwa kwa familia hiyo,” kilinyetisha chanzo hicho. Chanzo hicho kilishusha madai mazito kwamba, hivi karibuni baada ya ...