Ali Kiba na Hasheem wagongana kumuoa Jokate! Mkasa upo ha
mastaa katika category tofauti, Ali Saleh Kiba na Mtanzania anayecheza
mpira wa kikapu nchini Marekani (NBA), Hasheem Thabit Manka, wanadaiwa
kuchuana vikali kila mmoja akiwania kumuoa mwanamitindo Jokate Mwegelo
‘Kidoti’ huku mama mzazi wa mrembo huyo akitia ngumu, Risasi Jumamosi
linaweza kuripoti.
Chanzo
hicho kilishusha madai mazito kwamba, hivi karibuni baada ya Hasheem
kusikia tetesi za kushamiri kwa penzi la Kiba na Jokate, alidaiwa kukwea
pipa kutoka Marekani kisha akatua Bongo kimyakimya ambapo alifika
nyumbani kwa akina Jokate, Oysterbay jijini Dar ili kujua mbivu na
mbichi.
Habari za
awali, zilizovujishwa na mtoa taarifa wetu ambaye ni rafiki wa karibu na
familia ya Jokate, juzi Jumatano zilieleza kwamba, kwa sasa kuna vita
baridi kati ya Hasheem na Kiba kwa kila mmoja kutumia njia mbadala ili
kuhakikisha anamuweka kibindoni mrembo huyo.
MPASUKO NDANI YA FAMILIA
“Lakini
wakati hilo likiendelea, kuna taarifa kwamba kuna mpasuko kwenye familia
ya Jojo (Kidoti). Inasemekana mama wa mrembo huyo anampa nafasi kubwa
Hasheem.
“Lakini kwa upande wake, Jokate amekuwa akimnadi Kiba, jambo linalozua mpasuko mkubwa kwa familia hiyo,” kilinyetisha chanzo hicho.
“Lakini kwa upande wake, Jokate amekuwa akimnadi Kiba, jambo linalozua mpasuko mkubwa kwa familia hiyo,” kilinyetisha chanzo hicho.
“Baada ya
kuona hivyo, mama Kidoti aliitisha kikao cha dharura na kumtaka Jokate
akubali kuolewa na Hasheem ili waishi maisha mazuri lakini bidada
(Jokate) alilipinga vibaya na kushikilia alichokiita uhuru wa mapenzi na
kwamba chaguo lake ni Kiba.
“Kiukweli
hali mbaya sana kati ya Jokate na bimkubwa wake, mama anataka binti
aolewe na Hasheem lakini Jokate anashikilia msimamo wa kuwa na Kiba,”
kilinyetisha ‘kikulacho’ hicho.
Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
RISASI HADI KWA JOKATE
Ili
kung’amua lipi ni tui na yapi ni maziwa juu ya madai hayo, mwanahabari
wetu alisaga lami hadi ushuani, Oysterbay, Dar nyumbani kwa akina Jokate
ambapo aliwakuta watumishi wawili ambao walimwambia mwandishi wetu kuwa
Jokate na mama yake hawakuwepo, walitoka kwenda kwenye mihangaiko yao
ya kila siku.
UDADISI WAANZA
Ili kupata
chembechembe ya madai hayo, paparazi wetu alidodosa na kubaini kuwepo
kwa sintofahamu kati ya Jokate na mama yake huku jina la Hasheem
likitajwa kuwa alionekana maeneo hayo kama wiki mbili zilizopita.
JOKATE ‘BIZE’ MUDA WOTE
Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alimtafuta Jokate kupitia simu yake ya mkononi ambapo hakupokea licha ya kuita mfululizo.Hata alipotumiwa meseji kwa njia ya WhatsApp hakujibu licha ya kusomewa kila kitu.
Kwa upande wake, Kiba simu yake haikupatikana hewani huku Hasheem akielezwa amesharejea nchini Marekani.
Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alimtafuta Jokate kupitia simu yake ya mkononi ambapo hakupokea licha ya kuita mfululizo.Hata alipotumiwa meseji kwa njia ya WhatsApp hakujibu licha ya kusomewa kila kitu.
Kwa upande wake, Kiba simu yake haikupatikana hewani huku Hasheem akielezwa amesharejea nchini Marekani.
TUMEFIKAJE HAPA?
Kabla ya
kudaiwa kuwa mikononi mwa Mbongo-Fleva, Kiba, Jokate aliwahi kunasa
kwenye penzi la mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akitokea kwa
Hasheem ambaye ilidaiwa kwamba mrembo huyo alikufa kwake kiasi cha
kutaka kujiua baada ya kuachana naye.
Comments
Post a Comment