BREAKING NEWZ:SASA MAREKANI YATOA ANGALIZO UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA..SOMA KAULI YAO HAPA KALI
Siku moja tu baada ya Umoja wa Ulaya (EU) kutabiri kuwapo kwa ushindani
mkali katika uchaguzi mkuu nchini utakaofanyika Oktoba 25, Serikali ya
Marekani imeibuka pia na kutoa angalizo kuhusiana na uchaguzi huo
unaohusisha wagombea urais saba wakiwamo Dk. John Magufuli wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema).
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Shirika la Changamoto
za Milenia (MCC) linalomilikiwa na Serikali ya Marekani kwa ajili ya
kusaidia nchi zinazoendelea, ilieleza kuwa Bodi ya MCC ina matumaini
uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika Oktoba 25 utakuwa huru na wa
haki, hasa ikizingatiwa umuhimu mkubwa ambao MCC inauweka katika haki za
kidemokrasia.
Kadhalika, taarifa hiyo imemkariri Balozi wa Marekani nchini, Childress
akisema (Marekani) wanatambua rekodi ya Tanzania katika kukuza
demokrasia na kwamba, wanaunga mkono na kusaidia jitihada endelevu za
Tanzania katika kuimarisha taasisi zake za kidemokrasia.
“Tunatarajia kuona uchaguzi ulio huru, wa haki, wa amani na ambao
utawasilisha matakwa ya watu wa Tanzania,” alisema Balozi Mark
Childress.
Taarifa hiyo ya Marekani kuhusiana na uchaguzi mkuu nchini inatokana na
mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi ya MCC iliyokutana juzi kujadili masuala
mbalimbali yakiwamo ya utoaji wa misaada kwa Tanzania.
Mbali na Dk. Magufuli na Lowassa anayewakilisha pia muungano wa vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NCCR-Mageuzi, NLD na
Chama cha Wananchi (CUF), wagombea wengine wa nafasi ya urais
wanaoendelea na kampeni kwa nia ya kumrithi Rais Jakaya Kikwete ni Fahmy
Dovutwa wa UPDP, Hashim Rungwe wa Chaumma, Anna Mghwira wa
ACT-Wazalendo, Chifu Lutasola Yemba wa ADC

Comments
Post a Comment