Baada ya kununua Prado, Nay wamitego aasema ‘kinachofuata ni Range Rover’

Nay wa Mitego amesema akimaliza ujenzi wa nyumba yake mpya ya kifahari iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam, atanunua gari aina ya Range Rover.

Nay ambaye amenunua gari mpya, Prado Land Cruiser hivi karibuni, ameiambia Bongo5 kuwa lengo lake ni kumiliki Range.

“Bado sijapata gari ninayoihitaji, mpango wangu ni Range nikimaliza nyumba yangu ya Tabata,” alisema Nay.

“Hii Prado ni mpya lakini ina kazi maalum. Hii ni kwaajili shows za mikoani. Nimenunua milioni 60, ni mpya kabisa ndio maana unaona hata namba haina ila ikikamilika kila kitu itakuwa barabarani soon.

Comments

Popular posts from this blog

Ang'atwa na Nyoka Akizini na Mke wa Mtu Kichakani

Kubenea Aibua Ufisadi wa Billion 1.2 Kupitia Ufuaji wa Majoho ya Madiwani

Tundu Lissu Ajibu Mapigo.......Asema Mwenye Richmond ni Rais Kikwete Mwenyewe