MBUNGE wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea ameibua ufisadi wa Shilingi bil. 1.2 kwa mwaka katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam unaofanywa kupitia ufuaji wa majoho ya madiwani. Kubenea amesema hayo Stendi Kuu ya mabasi yaendayo mikoani alipofanya ziara ya siku moja kutembelea soko la Urafiki maarufu kama Mahakama ya ndizi, soko la Mabibo na kuhitimisha ziara yake katika Stendi za Ubungo na Simu 2000 “Baada ya kufanya uchunguzi tumebaini kuwa mradi huo wa ufuaji majoho kabla ya madiwani kufanya kikao unaotumia shilingi bilioni 1.2 hivyo basi Halmashauri ya Manispaa itakayokuwa chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) tukianza kazi tutaufuta,” alisema Kubenea. Aliongeza kuwa kufutwa kwa mradi huo kutafanywa mara moja baada ya Ukawa kupata Meya wa Manispaa na Jiji kutokana na ukweli kwamba wana Halmashauri mbili kati ya tatu hivyo zitawawezesha kumpata Naibu Meya katika Chama Cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Kubenea alisema jambo jing...
Wednesday, September 16, 2015 Siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amtaje mhusika wa Richmond anayezunguka naye kwenye kampeni, Mbunge huyo wa Singida Mashariki ameibuka na kudai kuwa Rais huyo ndiye mhusika kwa kuwa ndiye mwenye mamlaka ya kuteua na kuwawajibisha mawaziri. Juzi, akiwa Kigoma, Rais Kikwete alieleza kumshangaa Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mtu huyo anazunguka naye kwenye mikutano ya kampeni na kumtaka amtaje la sivyo yeye (Rais), atamtaja. Akihutubia mkutano wa kumnadi mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, mwanasheria hiyo alianza kwa kusema: “Sasa ndugu zangu naomba leo nimjibu Kikwete na tumalizane na hii habari ya Richmond." Alisema mkuu huyo wa nchi ndiye mhusika kutokana na mamlaka yake na; “si ya huyu Lowassa anayedai natembea naye kwenye kampeni. Hapa kwenye mkono wangu nina taarifa ya mwaka 2008 ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Richmond,...
Mwezi mmoja toka Jacqueline wolper atamke kuwa ni mjamzito (ambao bado haujapata uthibitisho-Ingia hapa ), mrembo huyo wa Bongo movie amevishwa pete ya uchumba. Kwa mujibu wa picha na maelezo aliyopost kwenye akaunti yake ya Instagram, Wolper sasa ni mchumba wa mtu. Wolper alipost picha kadhaa akiwa na mchumba wake, na kuelezea picha kamili ilivyokuwa hadi kupata surprise hiyo ambayo hakuitarajia. Baada ya maelezo hayo yaliyofatiwa na picha za tukio lenyewe, pongezi nyingi zimemwagika kutoka kwa followers wake. Hizi ni baadhi ya comments; annietzdu : Nakupongeza kwa kutochukua mtu maarufu mungu awatangulie sana mtimize lengo lenu mmeendana sana new_isha : Usiishie Pete ndoa fastaaa my nduguuuu love uuuu na unialike mwezimbili : Hongera kaka kwan umembadilisha tabia Dada Jack.hususanani ktk mavazi Mungu amibariki.Dada Jack jitambue kuna ile SKU moja utakua mama hivyo basi heshima ndio nguzo pekee ktk masha hebu onyesha mfano. beibycso :...
Comments
Post a Comment