Kubenea Aibua Ufisadi wa Billion 1.2 Kupitia Ufuaji wa Majoho ya Madiwani
MBUNGE wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea ameibua ufisadi wa Shilingi bil. 1.2 kwa mwaka katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam unaofanywa kupitia ufuaji wa majoho ya madiwani. Kubenea amesema hayo Stendi Kuu ya mabasi yaendayo mikoani alipofanya ziara ya siku moja kutembelea soko la Urafiki maarufu kama Mahakama ya ndizi, soko la Mabibo na kuhitimisha ziara yake katika Stendi za Ubungo na Simu 2000 “Baada ya kufanya uchunguzi tumebaini kuwa mradi huo wa ufuaji majoho kabla ya madiwani kufanya kikao unaotumia shilingi bilioni 1.2 hivyo basi Halmashauri ya Manispaa itakayokuwa chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) tukianza kazi tutaufuta,” alisema Kubenea. Aliongeza kuwa kufutwa kwa mradi huo kutafanywa mara moja baada ya Ukawa kupata Meya wa Manispaa na Jiji kutokana na ukweli kwamba wana Halmashauri mbili kati ya tatu hivyo zitawawezesha kumpata Naibu Meya katika Chama Cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Kubenea alisema jambo jing...


Comments
Post a Comment