Posts

;Biashara ya Maduka ya Dawa Baridi Muhimbili Yavurugwa

Image
BIASHARA ya maduka ya dawa baridi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeingia shubiri, huku maduka mengine katika hospitali za Serikali yakitakiwa kuwa tayari baada ya agizo la Rais John Magufuli, kuanza kutekelezwa.    Dk Magufuli alipoingia madarakani tu, moja ya maagizo yake alitaka Bohari ya Dawa (MSD) kufungua maduka ya dawa za Serikali kwenye hospitali za rufaa na za kanda, ambapo kesho kutwa Jumatatu duka hilo litaanza kufanya kazi Muhimbili na bei za dawa zitakuwa chini ya bei ya soko. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laureane Bwanakunu, amesema kufunguliwa kwa duka hilo kutaenda sambamba na kufunguliwa na duka lingine katika Hospitali ya Kanda ya Mbeya na baadaye kwenye hospitali zingine za rufaa na kanda na yatatoa huduma mpaka kwa wanaotumia utaratibu wa bima ya afya. Kwa mujibu wa Bwanakunu, pia MSD imeanza kuweka nembo ya Serikali kwenye vidonge na hadi sasa ina vidonge 45 ambavyo vimewekewa nembo ya GOT, ili ...

;Diamond: Sitaki Kabisa Kushika Simu ya Zari Naogopa Kuumia

Image
Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa yeye na mpenzi wake Zari ni watu ambao huwa hawapendi kupekuliana simu simu zao ili kuepukana na matatizo yanayoweza kusababishwa na simu za mikononi. Simu za mikononi huwa ni moja ya chanzo cha ugomvi kwa wapenzi wengi, na tumekuwa tukisikia story za couple nyingi kuingia kwenye matatizo kutokana tu na mmoja kukuta ujumbe au picha zenye utata kwenye simu ya mwenzie hata kama haimaanishi kuwa anamsaliti. Diamond na Zari wote ni watu maarufu ambao wana mashabiki wa jinsia tofauti, hivyo kwa kutambua mazingira ya kazi zao wameona ni bora kuaminiana bila kupekuana kwenye simu zao. “Hicho ni kitu cha kwanza ambacho siwezi kudiriki kabisa,” alijibu Diamond alipoulizwa na Millard Ayo kama huwa anashika simu ya Zari. Diamond aliendelea kutoa sababu za kutoshika simu yake, “sidiriki kwasababu namjua ni binadamu , unajua sometimes ukizingatia na yeye (Zari) ni mtu maarufu so sometimes watu wengine wanakuwa wanamsumbua, anaweza kukutwa na vishawishi some...

Waziri Mkuu akutana na hasara ya Bilioni 80 Bandarini

Image
Huko tunakokwenda naona minyukano live.......mie simoooo kazi yangu nafikisha habari tujadiliane.... . . "Siku moja tu ya ziara Waziri Mkuu amekutana na hasara ya Bilioni 80 Bandarini. Hizi ni fedha ambazo zinatosha kuwapa mkopo wa biashara vijana 40,000 wa Kitanzania kila mmoja akapata milioni 2. Pia zinaweza kujenga mabunge mawili yenye hadhi sawa na bunge la Dodoma na zikabaki Bilioni 10 (Bil 35 x 2). Ni fedha ambazo ukiziweka katika noti za elfu kumikumi unaweza kuzitandaza umbali wa kilomita 960 (Bil 80 ÷10,000/= × 12 ÷100,000). Kilomita 960 ni umbali wa kutoka Tunduma hadi Dar. Yani ukatandaza elfu 10 kutoka Tunduma, Mbeya, Makambako, Iringa, Mikumi, Moro hadi Dar bila kuacha hata sentimita moja njiani. Halafu tunaambiwa hii wizara ilikua na Waziri. Tena maWaziri wawili walioitwa maJembe. Mwakyembe na Sitta kwa nyakati tofauti. What a shame?? Majembe wezi? MaJembe ya kupiga dili na watu wa TRA? MaJembe yamekaa wizarani miaka mitano yakashindwa kuona Bil.80 zikipotea, Maj...

Kasi ya Rais Mgufuli, mzigo wa thamani zaidi ya milioni 300 wakamatwa bandarini.

Image
Kutokana na Kasi ya Rais Magufuli yenye motto wa HapaKaziTu, watendaji wa taasisi mbali mbali wameanza kuamka kwenye usingizi wa uzembe na kuanza kufanya kazi. Makontena zaidi ya 30 yamekamatwa yakiwa mbioni kusafirishwa kwenda nchini China yakiwa na mzigo wa magogo kinyume na sheria za nchi. Haijulikana makontena mengine mangapi yamesafirishwa kabla ya haya makontena kukamatwa. It's a new dawn, new day and new life for business as usual!

Sijapenda Majibu ya Msanii wa Diamond Harmonize Kuhusu Mimi- Rose Ndauka

Image
Rose Ndauka Msanii Rose Ndauka amesema kitendo cha msanii Harmonize kujibu majibu yenye utata alipokuwa akihojiwa na kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Televisio, hakupendezwa nacho kwani kinazidi kuleta sintofahamu. Rose Ndauka ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba Harmonize alitakiwa kujibu moja kwamoja kuwa hawana mahusiano yoyote zaidi ya kufahamiana nae kikazi. “Mi Harmonize namfahamu kama msanii, na hii issue sio mara ya kwanza, tayari nilishaona alihojiwa kwenye interview nyingine alihojiwa kuhusu mimi, what I didn't like ni kwamba angeongea straight, unajua kama huna mahusiano na mtu na ukaulizwa unaongea moja kwa moja, kitendo cha kutengeneza mazingira na watu wakaanza kuweka doubt kwamba Rose na Harmonize watakuwa na mahusiano, hicho ni kitu ambacho mimi sikukipenda”, alisema Rose Ndauka. Rose Ndauka aliendelea kwa kusema kwamba yeye na Haronize hawana mahusiano kama ambavyo H...

Dk. Manyaunyau Ahukumiwa Jela Miaka 3 Kwa Kushindwa Kufufua Maiti

Image
Mkazi  wa Dar es Salaam, Dunia Salumu maarufu kwa jina la Dk. Manyaunyau, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela pamoja na kulipa fidia ya Sh milioni 10 baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha Sh milioni 29.6 kwa njia ya udanganyifu. Manyaunyau anadaiwa kujipatia kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mlalamikaji, Tekra Modesta kama malipo ya kazi ya kumfufua marehemu kaka yake aliyefahamika kwa jina moja la Modest ambaye alifariki dunia miaka kadhaa iliyopita. Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Flora Haule, alisema mtuhumiwa huyo ametiwa hatiani baada ya ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka kujitosheleza. “ Mahakama inatoa hukumu kwa mtuhumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa fidia ya Sh milioni 10 baada ya kumaliza kutumikia kifungo chake ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo, ” alisema Hakimu Flora. Upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi wanne ambao wote waliithib...

Marekani Yaipa Kibano Tanzania .....Yaitaka Serikali itoe Maelezo Uchaguzi Zanzibar na Sheria ya Mtandao , Yatishia kusitisha Msaada wa Trilioni

Image
Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) wa Marekani umeonya kuwa hali ya kisiasa Zanzibar na tukio la hivi karibuni la watu kukamatwa chini ya sheria mpya ya uhalifu mtandaoni yanaweza kuathiri vigezo vya kuiwezesha Tanzania kupata msaada. Katika barua ya MCC ya Novemba 19, ambayo imesainiwa na Naibu Makamu wa Rais wa Idara ya Operesheni ya Miradi kwa Afrika, Jonathan O. Bloom kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile, mfuko huo umetaka maelezo kuhusu utatuzi wa mgogoro wa Zanzibar pamoja na ufafanuzi wa sheria ya uhalifu wa mtandaoni. “MCC inashukuru kwa uongozi na dhamira yako wakati wa mchakato mzima wa maendeleo ya mradi huu. Msaada wa dola milioni 472 (ambazo ni zaidi ya Sh trilioni moja), una nafasi kubwa ya kusaidia kuleta mageuzi katika sekta ya nishati na kuwaunganisha maelfu ya watu katika gridi. “Lakini mgogoro wa Zanzibar na ukamataji watu wa hivi karibuni kupitia sheria mpya ya uhalifu mtandaoni umetutia wasiwasi. “Kama ujuavyo, mataifa wa...