Hii sasa ni vita Zari, wema wapambana
Wema Isaac Sepetu. DAR ES SALAAM: Hii sasa ni vita! Mpambano mkali umeibuka kwa mara nyingine kati ya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu na nyota wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Uganda, The Boss Lady’ ambaye pia ni mzazi mwenzake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Mapambano hayo yameanzia kwenye mitandao ya kijamii kisha kuhamia mitaani kwa timu zao ambapo baadhi ya watu wanasema kuna kitu zaidi katika chuki ya Zari kwa Wema. KUTOKA MTANDAONI Ni Zari ambapo inadaiwa, mapema wiki hii alitupia kwenye akaunti yake ya Instagram maneno yaliyotafsiriwa ni kejeli kwa Wema. Aliandika: Fake car (gari magumashi), fake house (nyumba magumashi), fake men (wanaume magumashi). Zari Hasan The Boss Lady’. Kisha akatupia ujumbe akijifanya anawasiliana na wifi yake, yaani dada wa Diamond aitwaye Esma Platnumz akimuuliza: Umelipa Tanesco? Wema aliwahi kudaiwa kuchezea mita ya Luku ya Shirika la Umeme (Tanesco) hivyo kusababisha deni la shilingi mi...